Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Viwanja vya Mnara wa Mashujaa wa Vita ya
Majimaji, Mjini Songea, kushiriki uwekaji wa silaha za jadi kama ishara ya
kumbukizi ya Miaka 120 ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji. Tarehe 27 Februari
2026, Ruvuma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi akivalishwa skafu maalum na Chifu wa Kabila la Wangoni (Inkosi
ya Makhosi) Emmanuel Zulu Gama, wakati akiwasili katika Viwanja vya Mnara wa
Kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji, Mjini Songea, kushiriki uwekaji wa
silaha za jadi kama ishara ya kumbukizi ya Miaka 120 ya Mashujaa wa Vita ya
Majimaji. Tarehe 27 Februari 2026, Ruvuma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Makumbusho ya
Majimaji, Bi. Rose Kangu kabla ya kuweka silaha za jadi kwenye Mnara wa
Mashujaa wa Vita ya Majimaji, ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 120 ya Mashujaa wa
Vita ya Majimaji, iliyofanyika Songea, mkoani Ruvuma, leo tarehe 27 Februari
2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi akiweka silaha za jadi kwenye Mnara wa Mashujaa wa Vita ya
Majimaji ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 120 ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji,
iliyofanyika Songea, mkoani Ruvuma, leo tarehe 27 Februari 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua katika kaburi la halaiki la Mashujaa 66
wa Vita ya Majimaji ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 120 ya Mashujaa wa Vita ya
Majimaji, iliyofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Vita ya Majimaji
Songea, mkoani Ruvuma, leo tarehe 27 Februari 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua katika kaburi la Nduna Songea Mbano,
ambaye alikuwa kiongozi mwandamizi wa Mashujaa wa Vita ya Majimaji ikiwa ni
kumbukizi ya Miaka 120 ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji, iliyofanyika katika
viwanja vya Makumbusho ya Vita ya Majimaji Songea, mkoani Ruvuma, leo tarehe 27
Februari 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi akiweka silaha za asili kwenye Mnara wa Askari wa Vita ya
Majimaji ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 120 ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji,
iliyofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Vita ya Majimaji Songea, mkoani
Ruvuma, leo tarehe 27 Februari 2026.