Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap, akishirikiana na Askofu Msaidizi Henry Mchamungu, leo Februari 27, 2026 wamewaongoza Mapadre kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Polycarp Pengo (1944–2026) ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Ibada hiyo imehudhuriwa na mamia ya waumini, viongozi wa dini na serikali, waliokusanyika kumuombea na kumuenzi Kardinali Pengo kwa mchango wake mkubwa katika Kanisa na taifa kwa ujumla.
Sala, nyimbo za maombolezo na ibada maalum zimeongoza tukio hilo la kihistoria lililojaa simanzi na heshima kubwa kwa kiongozi huyo wa muda mrefu wa Kanisa Katoliki Tanzania.
