EWURA NA MISA TANZANIA WAUNGANISHA NGUVU KUIMARISHA UANDISHI WA HABARI ZA NISHATI NA MAJI

Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Lorivii Long’idu, akifungua warsha ya tathmini ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari kuhusu majukumu ya EWURA.

Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko akizungumza wakati wa warsha ya tathmini ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari kuhusu majukumu ya EWURA.

Na Kadama Malunde, Dar es Salaam

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwa kushirikiana na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania (MISA Tanzania), imeendesha warsha ya tathmini ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya mafunzo yaliyofanyika Juni 16, 2025.

Warsha hiyo imefanyika Februari 27, 2026 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Sea Shells Hotel, ikiwakutanisha wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa lengo la kupima mafanikio ya mafunzo ya awali na kuweka mikakati mipya ya kuimarisha ushirikiano kati ya EWURA na vyombo vya habari katika kuhabarisha umma kuhusu sekta za nishati na maji.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mhandisi Lorivii Long’idu, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, amesema vyombo vya habari vina nafasi ya kimkakati katika kuelimisha wananchi kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo, ikiwemo udhibiti wa bei, utoaji wa leseni, usimamizi wa ubora wa huduma pamoja na kushughulikia malalamiko ya watumiaji.

Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Lorivii Long’idu.

Ameeleza kuwa kuwajengea uwezo waandishi ni sehemu ya mkakati mpana wa EWURA wa kuhakikisha taarifa zinazotolewa kwa umma zina usahihi, uwiano na zinaakisi hali halisi ya utendaji wa sekta.

 “Tunaamini tukiwajengea uwezo waandishi wa habari, tunakuwa tumeifikia jamii kwa upana zaidi. Mnapoelewa vizuri tunachokisimamia, mnakuwa daraja sahihi kati ya EWURA na wananchi,” amesisitiza.

Mhandisi Long’idu amebainisha kuwa kwa mujibu wa takwimu za sekta ya nishati nchini, huduma zimeendelea kuimarika kwa ubora na upatikanaji, huku akiwahimiza waandishi kuandika habari za kuelimisha umma kuhusu haki na wajibu wa watumiaji. 

Amesisitiza kuwa malalamiko yote yanayowasilishwa rasmi katika ofisi za EWURA hushughulikiwa bila gharama yoyote, na kutoa mfano wa changamoto zinazojitokeza kwa baadhi ya wamiliki wa magari wakati wa ununuzi wa mafuta, pamoja na bili bandikizi za maji au umeme.

Aidha, amewataka waandishi kusaidia kuelimisha wananchi kufuata taratibu sahihi za kuwasilisha malalamiko yao badala ya kubaki na malalamiko yasiyo rasmi, akieleza kuwa utaratibu uliowekwa na EWURA unalenga kulinda maslahi ya watumiaji na kuhakikisha watoa huduma wanatekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kanuni.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema warsha hiyo ni muendelezo wa ushirikiano imara kati ya taasisi hizo mbili, akibainisha kuwa tangu kufanyika kwa mafunzo ya awali, jumla ya habari 103 zimeandikwa na kurushwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari zikihusu masuala ya udhibiti wa nishati na maji.

Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko.

Amesema mafanikio hayo yanaonesha umuhimu wa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi ili kuibua waandishi mahiri (champions) wenye uwezo wa kufanya uchambuzi wa kina, kuzingatia maadili ya taaluma na kuandika habari zenye kuleta suluhisho kwa jamii.

Soko ameishukuru EWURA kwa kuendelea kuiamini MISA Tanzania katika kuwajengea uwezo wanahabari na kuahidi kuwa waandishi waliopata mafunzo wataendelea kuwa mabalozi wazuri wa masuala ya udhibiti wa nishati na maji, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa karibu na ofisi za kanda za EWURA ili kupata taarifa sahihi na za kina.

Naye Afisa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa EWURA, Wilfred Mwakalosi, amesema bado kuna changamoto ya uelewa mdogo kwa baadhi ya wananchi kuhusu haki na wajibu wao katika matumizi ya huduma za nishati na maji, hali inayochangia kutowasilishwa kwa malalamiko kwa wakati au kutofuatwa kwa taratibu sahihi za kupata huduma.

Afisa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa EWURA, Wilfred Mwakalosi.

Ameeleza kuwa kuongezeka kwa uelewa wa umma kutasaidia kupunguza migogoro kati ya watumiaji na watoa huduma, kuimarisha uwajibikaji na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma hizo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Warsha hiyo imehusisha majadiliano ya wazi, maswali na majibu kati ya washiriki na wataalamu wa EWURA, na kufikia maazimio ya pamoja yaliyolenga kuimarisha ubora wa uandishi wa habari za sekta ya nishati na maji, kwa kuzingatia usahihi wa taarifa, maadili ya taaluma na maslahi ya umma.

Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Lorivii Long’idu, akifungua warsha ya tathmini ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari kuhusu majukumu ya EWURA. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog