Kardinali Rugambwa Aongoza Makardinali Kutolewa Heshima za Mwisho Mwili wa Pengo

Global Publishers
February 27, 2026
0 Comments

Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, amewaongoza makardinali wenzake kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mwadhama Polycarp Pengo, aliyekuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Katika tukio hili la kihistoria, Kardinali Rugambwa aliongozana na Fridolin Cardinal Ambongo Besungu, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Kinshasa nchini Democratic Republic of Congo, pamoja na Antoine Kambanda, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Kigali nchini Rwanda, kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi aliyehudumu kwa uaminifu na mchango mkubwa ndani ya Kanisa Katoliki Tanzania na Afrika Mashariki.

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alifariki dunia Februari 19, 2026, alipokuwa akipatiwa matibabu katika Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI). Mazishi yake yamepangwa kufanyika Jumamosi, Februari 28, 2026, katika Kituo cha Hija Pugu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.