Benki ya Absa kuendelea kushiriki mikakati ya kuboresha ustawi na maendeleo endelevu ya watoto, familia na jamii nchini

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akishikana mikono na Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Tanzania, Bw. James Anditi, wakati wa uzinduzi rasmi wa Mkakati wa miaka mitano wa Jubilei (2026–2030) wa shirika hilo jijini Dar es Salaam jana, unaolenga kuboresha ustawi na maendeleo endelevu ya watoto, familia na jamii nchini. Ushiriki wa Benki ya Absa unaakisi dhamira ya benki hiyo kuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa kuiwezesha jamii kupitia ushirikiano wenye malengo mahsusi unaopanua fursa, kuimarisha ustahimilivu na kusaidia athari endelevu za kijamii kwa muda mrefu, kwa kuiwezesha Afrika ya kesho, kwa pamoja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Mkakati wa miaka mitano wa Jubilei (2026–2030) wa Shirika la World Vision  jijini Dar es Salaam jana, unaolenga kuboresha ustawi na maendeleo endelevu ya watoto, familia na jamii nchini. Ushiriki wa Benki ya Absa unaakisi dhamira ya benki hiyo kuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa kuiwezesha jamii kupitia ushirikiano wenye malengo mahsusi unaopanua fursa, kuimarisha ustahimilivu na kusaidia athari endelevu za kijamii kwa muda mrefu, kwa kuiwezesha Afrika ya kesho, kwa pamoja.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima (katikati, waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi kutoka World Vision, Benki ya Absa pamoja na wadau wengine wakati wa uzinduzi rasmi wa Mkakati wa Jubilei (2026–2030) wa shirika hilo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam jana, unaolenga kuboresha ustawi na maendeleo endelevu ya watoto, familia na jamii nchini. Ushiriki wa Benki ya Absa unaakisi dhamira ya benki hiyo kuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa kuiwezesha jamii kupitia ushirikiano wenye malengo mahsusi unaopanua fursa, kuimarisha ustahimilivu na kusaidia athari endelevu za kijamii kwa muda mrefu, kwa kuiwezesha Afrika ya kesho, kwa pamoja.