
Mkurugenzi wa Vyuo vya Excellent Msaada Balula akizungumza katika Mahafali ya Saba ya Chuo cha Afya cha Excellen Kibaha mkoani Pwani.
Na Mwandishi Wetu
CHUO cha Excellent Na Mwandishi Wetu Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Excellent kimesema wahitimu wa Chuo hicho watakwenda kuwa chachu katika kutumikia sekta ya afya kwa weledi kutokana na mikakati ya Chuo hicho kwa kuwa na vifaa vya afya vya kisasa vya kufundishia pamoja na wakufunzi wabobezi.
Akizungumza katika Mahafali ya Saba ya Chuo cha Excellent Kibaha Mkurugenzi wa Vyuo vya Excellent Msaada Balula amesema kuwa wahitimu waliohitimu wana weledi wa kwenda kutumika katika sekta ya afya katika fani walizozisomea.
Balula amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa vyuo vya Excellent wahitimu zaidi 1500 ambao wameingia katika soko la ajira na kupata ujumbe kuwa wanajituma na wenye weledi katika kuhudumia jamii.
Aidha amesema kuwa wazazi wawapeleke vijana wao katila vyuo vya excellent watapata elimu na mafunzo ya kuweza kuingia katika soko la ajira kwenye sekta ya afya kutokana na kyongezeka kwa mahitaji ya watalaam yaliyochagizwa na Serikali ya awamu ya sita kujenga Hospitali ,Zahanati, pamoja vituo vya afya.
Balula aliongeza kuwa sekta ya afya lina fursa ya wataalam kujiajiri na kuendelea kutoa mchango katika taifa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya zilizo bora.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya Saba Chuo cha Afya cha Excellent John George amesema kuwa serikali imewekeza katika hospitali ,Zahanati na Vituo vya Afya ambapo uwekezaji huo unahitaji wataalam kikiwemo chuo cha Excellent.
George amesema kuwa vyuo vya afya ikiwemo Excellent vinatoa mchango katika sekta ya afya katika kutoa huduma kwa wananchi.
Amesema Excellent imeweka mazingira ya kusomea yanayoendana na uhalisia na kufanya wanafunzi kupata utaalam unaohitajika wa kwenda kutumika sehemu za huduma za afya.
Mkuu wa Chuo cha Excellent Kibaha Dkt.Rorgers Ndihagati amesema kuwa wahitimu hao wameandaliwa kwa kwenda kutumikia jamii ya watanzania katika sekta ya afya.
Dkt.Ndihagati amesema kuwa Chuo kinategemea wahitimu kuwa mabalozi wa kutangaza sifa za chuo na kile wanachofanya kinaleta uhalisia wa ubalozi wao.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Mhitimu akitoa salamu kwa niaba ya wahitimu wenzake katika mahafali ya Saba ya Chuo cha Afya cha Excellent Kibaha.

Mkuu wa Chuo cha Afya cha Excellent Dkt.Rorgers Ndihagati akizungumza katika Mahafali ya Saba ya Chuo cha Afya cha Excellen Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Vyuo vya Excellent Msaada Balula akizungumza na waandishi wa habari katika Mahafali ya Saba ya Chuo cha Afya cha Excellen Kibaha mkoani Pwani.

