Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Mohamed Omar (kushoto) akiwa na Mwandishi wa vitabu vya Anatomia kutoka MUHAS, Profesa David Ngassapa, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Appolinary Kamuhabwa akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa vitabu vitano vya Anatomia katika hafla fupi iliyofanyika leo Februari 27, 2026, Dar es Salaam katika siku ya hitimisho la Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na MUHAS
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
SERIKALI imesisitiza dhamira yake ya kuendeleza ubunifu katika sekta ya afya, ikiitaka taasisi za elimu ya juu kubadili tafiti zao kuwa suluhisho za vitendo na zenye ushindani sokoni.
Serikali imeendelea kuonesha dhamira thabiti ya kuwekeza katika elimu ya sayansi na teknolojia, utafiti na ubunifu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya maendeleo ya taifa na mageuzi ya sera ya elimu. Hayo yamesemwa na Dkt. Hussein Omary, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wakati wa hafla ya kielimu na ubunifu iliyowakutanisha wanafunzi, watafiti na wadau wa maendeleo.
Akizungumza katika hafla ya kufunga Wiki ya Pili ya Ubunifu ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Februari 28, 2026 jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar, alisema ubunifu katika sekta ya afya ni nguzo muhimu katika kukabiliana na ongezeko la idadi ya watu, mabadiliko ya mifumo ya magonjwa pamoja na matarajio makubwa ya wananchi kupata huduma bora na nafuu.
Alisema ni lazima kuendelezwa kwa suluhisho za ndani zinazozingatia mazingira na uhalisia wa Tanzania, akizihimiza taasisi kuwekeza katika utengenezaji wa vifaa vya uchunguzi, mifumo ya kidijitali ya afya, teknolojia za dawa na mifumo madhubuti ya utoaji huduma
“Serikali, kupitia Wizara ya Elimu, imewekeza kwa vitendo. Mheshimiwa Rais ametoa fedha za kusomesha vijana 50 waliobobea katika masomo ya sayansi katika vyuo mahiri duniani. Hadi sasa vijana 16 tayari wameshapelekwa nje ya nchi, huku wengine 34 wakitarajiwa kwenda visiwani kwa ajili ya kuendelezwa katika ubunifu na utafiti,” alisema Dkt. Omary.
Aliongeza kuwa tayari serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni mbili katika miundombinu ya hosteli na shilingi bilioni 4.6 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kielimu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza ubunifu na kupunguza changamoto za kitaaluma katika elimu ya juu.
Kwa upande wa upatikanaji wa vitabu vya kufundishia, Dkt. Omary alisema serikali inaendelea kuhamasisha uandishi, uchapishaji na usambazaji wa vitabu vinavyokidhi muktadha wa Tanzania, hususan katika elimu ya juu. Alifafanua kuwa kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), serikali imetenga bajeti maalum kwa ajili ya kuandaa na kusafisha vitabu, kuanzia ngazi za chini huku maandalizi yakiendelea kuelekea elimu ya juu kwa ushirikiano na vyuo vikuu.
Hafla hiyo ilikuwa chini ya kaulimbiu isemayo, “Kuendeleza Ubunifu katika Afya: Kukuza, Kuunganisha na Kulinda Suluhisho kwa Afya Bora”, na ulihusisha maonesho ya teknolojia bunifu za afya, suluhisho zinazotokana na tafiti pamoja na ubunifu wa wanafunzi.
Sambamba na hafla pia, kulifanyika uzinduzi wa kitabu cha Profesa David Ngassapa, kilichoangazia uhusiano kati ya taaluma na ubunifu wa vitendo katika sekta ya afya.
Kwa upande wake, Profesa Appolinary Kamuhabwa, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), alisema chuo hicho kimeingia makubaliano na wadau mbalimbali wakiwemo CRDB Foundation ili kuvuta na kukuza ubunifu wa vijana.
Alisema bunifu nyingi tayari zimeanza kuingia sokoni, nyingi zikiwa zinalenga changamoto za kijamii kama afya ya uzazi, uchunguzi wa magonjwa, ajali na huduma za dharura.
“Zaidi ya asilimia 90 ya bunifu hizi zimetengenezwa na wanafunzi wetu na vijana. Kama chuo, tumetenga shilingi bilioni 35 katika mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kusaidia ubunifu na utafiti,” alisema Profesa Kamuhabwa, akiwapongeza wadau waliojitokeza kuunga mkono juhudi hizo.
Alisisitiza umuhimu wa vyuo vikuu na maprofesa kuandika vitabu vinavyoakisi mazingira ya Tanzania badala ya kutegemea vitabu vya nje ambavyo wakati mwingine havizingatii uhalisia wa nchi. Alisema MUHAS itaendelea kuhamasisha uandishi na uchapishaji wa vitabu vya ndani kama sehemu ya kutekeleza dira ya taifa ya miaka 25 ijayo.
Profesa Kamuhabwa alieleza kuwa mfumo wa ubunifu wa chuo hicho umekua kwa kasi na sasa unajumuisha suluhisho zilizo tayari kuingia sokoni kama Afya Lead, Pona Health, May Care na Saratani AI.
Alibainisha kuwa Wiki ya Ubunifu imepanuka kwa ukubwa na ubora, ikijumuisha maonesho, vipindi vya elimu kuhusu haki miliki, ushauri elekezi kwa wabunifu na uunganishaji na wawekezaji, jambo linaloonesha mkakati mahsusi wa kubadili mawazo kuwa suluhisho zenye manufaa kwa jamii.
Mwandishi wa vitabu vya Anatomia MUHAS, Profesa David Ngassapa akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika MUHAS leo Februari 27, 2026, Dar es Salaam katika siku ya hitimisho la Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na MUHAS iliyoenda sambamba na uzinduzi wa vitabu vitano vya Anatomia
Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika MUHAS leo Februari 27, 2026, Dar es Salaam katika siku ya hitimisho la Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na MUHAS.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika hafla ya kushiriki hitimisho la Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na MUHAS.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)