Global Publishers
March 2, 2026
0 Comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uhamisho na kupangua vyeo vya mabalozi katika vituo mbalimbali nje ya nchi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo unawahusisha mabalozi kadhaa waliopangiwa kuziwakilisha Tanzania katika mataifa na taasisi za kimataifa.
