Global Publishers
March 4, 2026
0 Comments
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) leo Machi 4, 2026 imetangaza bei kikomo zitakazotumika Machi mwaka huu.
Bei ya rejareja ya petroli jijini Dar es Salaam imeongezeka hadi Sh2,864 kwa lita kutoka Sh2,788 ya Februari, ikiwa ni ongezeko la Sh76.
Dizeli imepanda kwa kasi zaidi ikiwa na ongezeko la Sh157, ambapo itauzwa Sh2,858 kutoka Sh2,701, huku mafuta ya taa yakiongezeka kwa Sh186 ambapo itauzwa Sh2,932 kutoka Sh2,746.


