Na Neema Adrian Gpl
Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania imewaomba wapenzi wamichezo hiyo kushiriki mchezo wa kubahatisha kwani inaendelea kubadilisha maisha kupitia Jackpot, Kasino na Aviator.
Kampuni hiyo imesema wapenzi wa michezo ya kubahatisha nchini Tanzania, SportPesa Tanzania ni zaidi ya jukwaa la kubeti na ni sehemu ambayo inawawezesha wachezaji kupata fursa halisi kushinda na kuona matokeo yanayobadilisha maisha.
“Mwaka uliopita, kampuni hii ilitoa zaidi ya TZS 1 bilioni kwa wachezaji wa jackpot pekee, ishara inayoonesha kwamba ushindi halisi unapatikana kila siku. Miongoni mwa washindi wapya ni Hamza Athman, aliyejinyakulia kitita cha TZS 237,897,560 kwenye Midweek Jackpot. Kwa Hamza, pesa hizi si tu namba kwenye skrini, bali pia ni fursa mpya na mwanzo wa sura mpya ya maisha yake,” imesema taarifa yao.
Akizungumza baada ya kupokea zawadi yake rasmi, Hamza alisema: “Kushinda Midweek Jackpot kumebadilisha maisha yangu kabisa. Daima niliamini kuwa ukiwa unataka kushinda kweli, lazima uwe na App ya SportPesa. Leo naweza kusema kwa hakika SportPesa Tanzania ni nyumbani kwa washindi. Wanampa kila mtu fursa ya kushinda Zaidi.”
Ukiacha ushindi wa Jackpot, SportPesa Tanzania pia ina michezo ya Kasino na Aviator na imekuwa ikizalisha washindi kila siku, kila dakika kwa dau dogo kabisa.
“Mwezi huu pekee, mchezaji mmoja mwenye bahati kwa dau dogo kabisa la shilingi 420, aliweza kujishindia hadi kiasi cha shilingi 27,964,800. Hii inadhihirisha kuwa kila dau linaweza kukupa ushindi mnono,” imesema taarifa yao.

Taarifa yao imefafanua kuwa ushindi huo unathibitisha kuwa SportPesa Tanzania inatoa fursa kwa wachezaji kwa kiwango chochote, iwe ni jackpots zenye odd ndefu, ubashiri wa michezo, au Aviator yenye multiplier kubwa, wachezaji wanaendele kupata malipo yao na kuingia kwenye akaunti zao.
SportPesa Tanzania inafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na sheria za serikali, ikichangia kwa kiasi kikubwa kwenye mapato ya taifa na kutengeneza maelfu ya ajira. Pia inakuza mpira, vipaji, uwajibikaji na kulinda wachezaji. Hii inaonesha kuwa, zaidi ya ushindi, SportPesa inachangia pia katika ukuaji wa jamii na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Masoko wa SportPesa Tanzania, Tracy Humplick alisisitiza kuwa kampuni inaendelea kuwekeza katika maboresho ya mfumo, uzoefu wa wateja na kurahisisha masharti ya michezo ili kuhakikisha haki na uendelevu wa huduma .
“Kila siku, wachezaji wanapokea ushindi wao. Kwa dau dogo tu unaweka na kupata mamilioni. Ushindi wa jackpot, Kasino au Aviator, ni ushahidi wa kwamba SportPesa ni kweli nyumbani kwa washindi,” alisema.
“Hadithi za washindi kama Hamza zinahamasisha wengine kujiunga na nyumba hii ya washindi, na inaonyesha kuwa fursa halisi ipo kwa kila mchezaji anayejituma. Kadri watanzania wengi wanavyoshiriki, mzunguko wa fursa na malipo unapanuka zaidi,” alisema Humplick.