Waziri Mkuu Mwigulu Awasili Arusha Kuzindua Miradi ya Kilimo na Kuzungumza na Wananchi

Global Publishers
March 6, 2026
0 Comments

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Machi 6, 2026 amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja mkoani Arusha katika Wilaya za Karatu na Monduli.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anategemea kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa skimu za umwagiliaji katika Bonde la Eyasi, lililopo Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha.

Pia, Mheshimwa Dkt. Mwigulu atafanya mikutano ya hadhara Karatu mjini pamoja na Mto wa Mbu Wilayani Monduli