Dar es Salaam. Wadau wakiwamo wanawake zaidi ya 400 kutoka sekta mbalimbali nchini, wakishiriki Jukwaa la Sita la The Citizen Rising Woman Initiative (RWI) linalofanyika muda huu katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.
LIVE: The Citizen Rising Woman 2026
Jukwaa hili linafanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 na kaulimbiu yake inasema isemayo: “Give to Gain: Elevate Her Rise,” ikimaanisha: “Toa ili Upate: Inua Safari ya Mafanikio ya Mwanamke.”
Jukwaa hili linaloandaliwa kila mwaka na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), huwakutanisha wanawake na wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili uwezeshaji wa wanawake, kubadilishana uzoefu na kujenga mitandao ya kitaaluma.