Wanawake wa TRA Morogoro Wawafariji Watoto Yatima na Wazee

Kuelekea ya Siku ya Wanawake Duniani, wanawake wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro wametembelea na kutoa msaada katika kituo cha kulelea watoto yatima  RAYA, MGOLOLE  pamoja na kituo cha kulelea wazee cha Fungafunga kilichopo Manispaa ya Morogoro.

Ziara hiyo imelenga kuonyesha upendo, mshikamano na kuwafariji watoto pamoja na wazee wanaohitaji msaada katika jamii, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku hiyo muhimu kwa wanawake duniani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Maneja msaidizi Ukaguzi Beatrice Stephen amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa vitendo, kwa kushirikiana na jamii na kusaidia makundi yenye uhitaji maalum.

Katika ziara hiyo, wanawake wa TRA walitoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo chakula, mavazi pamoja na mahitaji mengine muhimu kwa watoto na wazee waliopo katika vituo hivyo.