Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imesikiliza maombi Na. yanayotokana na shauri la madai Na.8323/2025, maombi yaliyoletwa Mahakamani hapo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu
Wajibu maobi hapo ni wadaawa wote walioko kwenye shauri la madai Na. 8323/2025 linalohusu usawa kwenye mgawanyo wa mali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ndani ya CHADEMA ambao ni Saidi Issa Mohamed, Maulidah Anna Komu, na Ahmed Rashid Khamis ambao ni waleta maombi kwenye shauri la msingi
Sambamba na hao pia wapo Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA ambao kimsingi ni wajibu maombi kwenye shauri la msingi, linalosikilizwa mbele ya Jaji Hamidu Mwanga, ikumbukwe kuwa Lissu ambaye kwa sasa yuko gerezani kutokana na mashtaka ya uhaini yanayomkabili amefungua maombi hayo Novemba 14.2025 akiomba kujumuishwa kwenye shauri hilo kama sehemu ya wajibu maombi
Akizungumza Mahakamani hapo leo, Lissu ambaye kitaaluma ni Mwanasheria na Wakili mbobevu amesema maombi hayo yameletwa kwa njia ya chamber summons ikiungwa mkono na hati ya kiapo chake ya Desemba 12.2025, ambapo amesema hoja zinazounga mkono maombi hayo zitapanua ushahidi uliopo kwenye hati ya kiapo chake,
Lissu ameanza kwa kuzungumzia msingi wa kisheria wa maombi hayo ambapo amesema, hati ya maombi inaonesha wazi kuwa maombi hayo yameletwa chini ya masharti ya amri ya kwanza ya kanuni ya kumi (2) ya sheria ya mwenendo wa madai sura ya 33 ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo pamoja na vifungu vingine vya sheria husika inahusisha ‘reference to order 43 rule 2 of CPC’ inayoelekeza kwamba maombi yote kwa mujibu wa sheria hiyo lazima yawasilishwe Mahakamani kwa njia ya hati ya maombi yakiungwa mkono na hati ya kiapo cha muhusika
Amesema hoja ya msingi ipo katika amri ya kwanza ya kanuni ya pili ya sheria ambapo kupitia amri hiyo, Mahakama inaweza katika hatua yoyote ya mashauri, aidha kwa maombi ama bila maombi ya upande wowote na kwa masharti ambayo Mahakama itaona ni ya haki kuamuru kwamba jina la mdai yoyote limeongezwa kimakosa liondolewe, na kwamba jina la mtu yeyote ambaye amateakiwa kuunganishwa aidha kama mdai ama mdaiwa ama uwepo wake mbele ya Mahakama atatakiwa kuwa wa lazima ili kuiwezesha Mahakama kufanya uamuzi kwa ukamilifu/ ufanisi
Lissu ameieleza Mahakama kuwa kifungu hicho ndio msingi kama aliyosema Mahakamani hapo awali kuwa maombi hayo na kifungu hicho yanaipa Mahakama mamlaka yake ya kuamuru asiyepaswa kuwemo kwenye shauri husika aondolewe na aliyepaswa kuwepo lakini hayupo aingizwe kwa masharti ambayo Mahakama inaona ni haki ili kuiwezesha Mahakama kufanya kazi kwa usanifu
Pia kifungu hicho kinaipa mamlaka Mahakama kusikiliza na kuamua mashauri yote, sambamba na hilo ikumbukwe kuwa kifungu hicho cha mwenendo wa madai kimefanyiwa maamuzi mengi sana na Mahakama za juu, na kwamba kuna mnyonyoro mkubwa wa maamuzi juu ya kifungu hicho
Amesema mahitaji ya jambo hilo ni kuiomba Mahakama kuangalia inapokutana na maombi kama hayo, juu ya mtu anayetakiwa kuondelewa ama kuongezwa kama mdahawa
Katika kujenga hoja zake, Lissu ameialika Mahakama katika kesi ya Mussa Chande, Moza Mohammed Salim ambayo ni Civil Appeal 14, number 1, katika Mahakama ya rufani Zanzibar, kesi ya pili ni ya Stanbick Bank, Iddi Khalfan Na. 139/2021 ya Mahakama ya rufani Tanzania, Dar es Salaam
Amedai kuwa kupitia marejeo hayo imebainishwa kuwa mtu anayetakiwa aunganishwe uwepo wake ni wa lazima na bila yeye kuwepo amri ya mwisho ya Mahakama haiwezi kutolewa kwa ufanisi
Amesema Mahakama ya Rufani ilijiuliza inakuaje pale ambapo mtu huyo hajaunganishwa, ambapo kwenye hilo Mahakama ya Rufani ikasema ikarudi kwenye kesi ya TAN GAS kisha ikasema ‘its now and acceptable of the law for the court (falier is veto)’
Amedai kuwa ni kosa la msingi kutomuunganisha mdahawa katika kesi ya msingi, pia kutomuunganisha mdahawa kunaua kesi ya msingi (Veto), na katika hilo amerejea kesi ya Stanslaus Kanokola iliyoamuliwa na Mahakama ya Rufani ya Tanzania
Amesema kama ilivyo katika maombi yake, wajibu maombi wa kwanza, pili na watatu wameshikilia uzi kwamba mleta maombi asiingiie, hivyo kuhoji inakuaje kwamba wadahawa wanasema huyo asiingie wakati ni muhusika?, katika majibu yame amesema sheria haina ubishi tena pale Mahakama inapogundua kwamba mdahawa hajaunganishwa katika kesi na pande husika hazijaomba aunganishwe, Mahakama ina wajibu tofauti na huo wa kutowakubalia na kuamuru aunganishwe