Arusha. Rais wa Rwanda, Paul Kagame na wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Félix Tshisekedi hawajawasili jijini Arusha zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mkutano wa 25 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Katika mkutano huo jumla ya wakuu wa nchi wanane walitarajiwa kuhudhuria lakini, Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva amesema marais hao hawatakuwepo kutokana na kuzidiwa na majukumu ya ndani ya nchi.
Amesema marais hao wamewasilisha taarifa rasmi wakieleza kuwa ratiba zao za kazi na majukumu mengine ya kitaifa vimewazuia kushiriki moja kwa moja katika mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa AICC.
Kwa upande wa Rais Kagame, Nduva amesema amewasilisha ujumbe wa kuomba radhi akieleza anakabiliwa na mgongano wa ratiba pamoja na majukumu mengine ya kikazi huku Tshisekedi akiteua mawaziri wawili kuiwakilisha nchi yake katika mkutano huo.
Endelea kufuatilia Mwananchi