Moshi unafuka baada ya shambulizi la anga huko Beirut, Lebanon.
Habari za Umoja wa Mataifa
Ghasia kote Mashariki ya Kati zinaendelea huku mashambulizi ya kijeshi na mashambulizi ya kukabiliana yakiripotiwa katika nchi kadhaa katika eneo hilo, na kuzua hofu ya kukosekana kwa utulivu na kuzorota kwa hali ya kibinadamu. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa mzozo huo unaathiri nchi zisizopungua 16, huku vifo vya raia, kuhama na uharibifu wa miundombinu muhimu ukiongezeka. Fuata matangazo yetu ya moja kwa moja kwa sasisho na majibu kutoka kwa mfumo wa Umoja wa Mataifa. Watumiaji wa programu ya UN News wanaweza kufuata hapa.