Global Publishers
March 7, 2026
0 Comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Machi 7, 2026 ameshiriki katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Jijini Arusha.

Mkutano huu umewaleta pamoja viongozi wa nchi wanachama wa EAC kujadili masuala muhimu ya kikanda, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya uchumi, usalama wa kanda, na ushirikiano wa kibiashara. Ushiriki wa Rais Samia unaashiria umuhimu wa Tanzania katika kuendeleza ajenda ya EAC na kudumisha mshikamano wa kikanda.

