Profesa Wa Sheria, Mwanadiplomasia Costa Mahalu Afariki Dunia Akiwa na Umri wa Miaka 77

Bakari Mahundu
March 9, 2026
0 Comments

 

Profesa wa sheria na mwanadiplomasia, Costa Mahalu (77), amefariki dunia.

Taarifa kutoka kwa familia yake imethibitisha kuwa Profesa Mahalu amefariki leo Jumatatu, Machi 9, 2026, katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), alipokuwa akipatiwa matibabu.

Profesa Mahalu alitambuliwa kama msomi mahiri, mwalimu mwenye bidii na mwanadiplomasia mwenye uzoefu, aliyetoa mchango mkubwa katika kukuza taaluma ya sheria na kuimarisha uwakilishi wa Tanzania katika medani za kimataifa. Alizaliwa Julai 9, 1948, katika Kijiji cha Katunguru, Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza.