Global Publishers
March 10, 2026
0 Comments
Kiongozi wa kijeshi wa Madagascar, Kanali Michael Randrianirina, amevunja serikali nzima kwa kumfuta kazi Waziri Mkuu pamoja na mawaziri wote wa baraza la mawaziri katika hatua ya kushtukiza.
Taarifa kutoka kwa msemaji wake imesema serikali imeacha rasmi kutekeleza majukumu yake, huku Randrianirina akitarajiwa kumteua Waziri Mkuu mpya na kuunda baraza jipya la mawaziri.
Randrianirina alichukua madaraka Oktoba mwaka jana baada ya maandamano makubwa yaliyoongozwa na vijana kupinga uhaba wa umeme na maji, hali iliyosababisha jeshi kumuondoa madarakani aliyekuwa rais Andry Rajoelina.
Hatua hii mpya inaongeza mvutano wa kisiasa nchini humo wakati Madagascar ikiendelea na kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi mpya uliopangwa kufanyika ndani ya miaka miwili.