Harakati za Muqawama zimetoa taarifa zikilipongeza taifa la Iran kwa mnasaba wa kuchaguliwa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kama Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imempongeza Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kwa kuchaguliwa kwake kama Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ikisisitiza kwamba, kundi hilo Kiongozi la Mapambano ya Kiislamu litaendelea kwa karibu na Jamhuri ya Kiislamu.
Katika taarifa yake, Hizbullah imetangaza utiifu wake kwa Ayatullah Mojtaba Khamenei, ikieleza kuwa itafuata amri zake kama Faqii Mtawala, sambamba na kuufanya utawala mtenda jinai wa Marekani ujutie uvamizi na chokochoko zake.
Aidha Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetoa taarifa ikipongeza mchakato mzuri na laini wa kukabidhi mamlaka nchini Iran, ikieleza kuwa hatua hiyo inaashiria kuwa madhubuti mfumo wa uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu.
Mohammed Ali al-Houthi, mwanachama wa Baraza Kuu la Uongozi la Yemen amesema makabidhiano ya madaraka yaliyofanyika Iran yanaonesha namna wananchi wa Iran wana umoja, utangamano na daima kuwa tayaari kusimama kidete kupigania mfumo na taifa.
Kadhalika Abu Hussein Al-Hamidawi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Kataib Hizbullah ya Iraq sanjari na kumpongeza Ayatullah Mojtaba Khamenei kwa kuchaguliwa kwake, imemtaja shakhsia huyo kama Kiongozi mpya na mbeba bendera ya Muqawama duniani.
Amemtaja Ayatullah Mojtaba Khomeini kama kiongozi mwenye ustahiki na sifa zote za uongozi, akimueleza kama shakhsia mwenye tajriba ya kubeba jukumu linalomwajihi katika kipindi hiki kigumu na hasa.
Hali kadhalika Muungano wa Vijana wa Harakati ya Februari 14 ya Bahrain umempongeza Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ukisema kuwa unataraji uteuzi huo utaimarisha umoja wa Waislamu na mrengo wa Muqawama duniani.