Tanzania yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Marburg

Ugonjwa huo ulioripotiwa kwa mara ya kwanza tarehe 20 Januari 2025 katika Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera ambapo watu wawili kutoka mkoani humo walithibitika kuwa na maisha na kupoteza maisha wakipatiwa matibabu.

Katika ripoti ya ripoti na Waziri wa Afya Jenista Mhagama imeeleza kuwa mgonjwa wa kwanza aliripotiwa tarehe 28 mwezi Machi 2025 siku 42 zilikamilika bila ya kuwa na maambukizi mapya, na hivyo kukidhi vyombo vya shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu kumalizika kwa mlipuko huo wa Marburg.

“Kitaalamu na kulingana na kanuni za Shirika la Afya Duniani WHO, tumekidhi vigezo vya kutangaza rasmi kumalizika kwa mlipuko wa Marburg. Hivyo basi, leo tarehe 13 Machi, 2025, nitatangaza rasmi kumalizika kwa mlipuko wa Marburg nchini.” Amesema Mhagama.

Abiria wakiwasili kupanda treni ya umeme inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma Augosti 1, 2024.

Wataalamu wa Afya nchini Tanzania wanasema licha ya kumalizika kwa ugonjwa huo, serikali ni kuboresha utoaji wa taarifa wakati kunapotokea magonjwa ya mlipuko kutokana na taarifa za kuwepo kwa ugonjwa huo huchelewa kutolewa na mamlaka.

Daktari wa Afya Betty Sanga kutoka Dar es Salaam anasema ni serikali kuendelea juhudi za utoaji wa taarifa ya elimu juu ya namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko kipindi chanapojitokeza.

“Juhudi za kusambaza taarifa za kuelimisha watu jinsi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko bado hazitoshi, kwahiyo kuna kazi kubwa ya kufanya mbele yetu kama taifa ili kuweza kumaliza na haya magonjwa ya mlipuko” Amesema Sanga.

Waziri wa Afya amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo licha ya kutangazwa kutangazwa kumalizika ni pamoja na kunawa kwa maji tiririka na sabuni, pamoja na kutoa taarifa za uvumi au tukio lolote lisilo la kawaida katika jamii.

Mtu akinawa mikono katika soko la Mabibo huko Dar es Salaam, Tanzania Aprili 16, 2020
Mtu akinawa mikono katika soko la Mabibo huko Dar es Salaam, Tanzania Aprili 16, 2020

Dkt Mugisha Ntiyonza rais wa Chama cha Madaktari Tanzania amepongeza jitihada zilizofanywa na wizara ya Afya, jamii, madaktari na vyombo vya kimataifa kwa usalama na kulinda Tanzania inakabiliana na ugonjwa huo.

“Ni hatua sana na kuongezwa katika sekta ya Afya Tanzania wote muhimu walioshiriki, Madaktari, watoa huduma, wananchi wa mkoa wa Kagera Jumuiya za kimataifa (WHO) na wengine wote walioshiriki katika mapambano haya pongezi sana” amesema Dkt Ntiyonza.

Aidha, Dkt Ntiyonza ameitaka kuboresha kuboresha mamlaka ya udhibiti ili kuleta utulivu kuwa nchi ya Tanzania inaendelea kuwa salama wakati wote.

Imetayarishwa na Amri Ramadhani Sauti ya Amerika.