Tanga. Wafanyakazi 471 wa kampuni moja katika mradi wa ujenzi wa gati la kupokelea mafuta baharini kwa ajili ya bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP), wamewasilisha malalamiko katika Kliniki ya Sheria jijini Tanga wakidai kutolipwa stahiki zao za kazi.
Kliniki hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inafanyika katika viwanja vya Tangamano, ilianza Machi 9, 2026 na inatarajiwa kumalizika Machi 15, 2026, ikiwa na lengo la kutoa msaada wa ushauri wa kisheria kwa wananchi bila malipo.
Wafanyakazi hao walifika katika kliniki hiyo tangu Machi 10, 2026 na kuwasilisha madai mbalimbali kwa mawakili wa Serikali wanaotoa huduma hiyo, wakitaka kupata mwongozo wa kisheria kuhusu stahiki zao kazini.
Akizungumza Machi 11, 2026 kwa niaba ya wafanyakazi hao, Elisafi Andasoni amesema mradi huo ambao umefikia takribani asilimia 90, umehusisha kazi ngumu baharini lakini baadhi ya wafanyakazi hawapati stahiki walizoahidiwa, ikiwemo posho ya mazingira magumu.
Andasoni amesema baadhi ya wasimamizi wa mradi na mameneja wa ujenzi wamekuwa wakiwajibu ovyo kwa kuwaambia ‘asiyetaka anaweza kuacha kazi na hawana mahali pa kukimbilia kudai haki zao.’
Amesema ndiyo maana wanachukua uamuzi ambao hauzingatii hali halisi ya kazi za wafanyakazi, jambo ambalo limekuwa chanzo cha malalamiko.
“Tunapouliza kuhusu stahiki zetu, mara nyingi wanajibu kuwa tunapaswa kufuata masharti ya mikataba tuliyoisaini, lakini mikataba hiyo haionyeshi hatari halisi tunayokabiliana nayo baharini,” alisema.
Amesema katika makubaliano ya awali walielezwa kuwa wangepatiwa huduma mbalimbali ikiwemo malazi, chakula, usafiri na matibabu, lakini hali halisi imekuwa tofauti na matarajio yao.
“Tunafanya kazi kwenye mazingira magumu baharini lakini huduma tunazopata hazilingani na tulichoahidiwa,” amesema Andasoni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Besix Ballast Nedam Limited (BBN) wanaofanya kazi katika mradi wa ujenzi wa gati la kupokelea mafuta baharini kwa ajili bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) wakisubiri kusikilizwa kwa shauri lao la mgogoro wa ajira katika kliniki ya sheria katika viwanja vya Tangamano.
Kwa mujibu wa mfanyakazi huyo, tofauti ya masilahi kati ya wafanyakazi wa ndani na wale wa kigeni wanaofanya kazi katika mradi huo imekuwa chanzo cha malalamiko.
Amesema wafanyakazi wa kigeni hupatiwa huduma bora zaidi, ikiwemo chakula na usafiri unaowafikisha hadi wanakoishi, wakati wafanyakazi wa ndani hulazimika kushuka mbali na makazi yao na kujitafutia usafiri kama bodaboda.
“Wenzetu wanafikishwa hadi mlangoni wanakoishi, lakini sisi tunashushwa njiani na kujitafutia usafiri kwa gharama zetu.”
Malalamiko mengine yanahusu malipo wanayopata wanapofanya kazi baharini, wakidai kuwa kazi hiyo ni hatarishi lakini malipo wanayopata ni madogo.
“Mtu mwingine akienda kufanya kazi kama hiyo analipwa zaidi ya Sh100, 000 kwa siku, lakini sisi tunapewa takribani Sh1, 000 tu,” alidai mfanyakazi mmoja.
Aidha, amedai mfumo wa bima ya afya waliyopewa baadhi ya wafanyakazi haukidhi mahitaji yao, hivyo wakati mwingine hulazimika kuchangia fedha zao ili kugharamia matibabu wanapougua au kujeruhiwa kazini.
Pia, amesema wamekuwa wakizunguka katika ofisi za mkuu wa mkoa ili kupata muafaka wa jambo lao lakini imekuwa ni shida na mara ya mwisho kukutana na mkuu huyo ni Jumatatu ya Machi 2, 2026 ambayo aliwataka kuwa wavumilivu kusubiri kliniki ya sheria.
Amesema wamekuwa wakigoma mara kadhaa na kukatwa malipo yao kutokana na migomo waliyofanya, jambo ambalo limekuwa likiwaumiza kwani wanakuwa wanadai haki zao za msingi.
“Tunaona wenzetu wanalipwa vizuri na chakula kizuri lakini sisi imefikia hatua tunakula chakula kibovu na mlo mara moja wakati wenzetu wanalipwa Sh8,000 kwa ajili ya chakula kwa siku,” amesema.
Aidha, Andasoni amesema masuala mengine ni pamoja na muda wa kazi unaofanywa kila siku na kwa wiki. Wafanyakazi wanafanya kazi kwa saa zaidi ya zilizopangwa, mara nyingine bila malipo ya muda wa ziada, ikiwemo Jumamosi.
“Wafanyakazi wa ndani wanashughulika na hatari kubwa, lakini baadhi ya stahiki na haki zinazostahili kulipwa hazitolewa. Hali hii inapelekea kutoeleweka na kutozingatia uwiano wa haki kazini,” alisema Andasoni.
Wafanyakazi hao wanasema walifika Kliniki ya Sheria kueleza changamoto hizi kwa mawakili wa Serikali, wakitarajia kupata mwongozo wa kisheria kuhusu hatua za kuchukua ili kudai haki zao kulingana na sheria za kazi.
Kwa mujibu wa Andasoni, wafanyakazi hao pia wamekuwa wakilalamikia mikataba ya ajira ambayo wamekuwa wakigomea mara kwa mara tangu 2023 na kuongezewa kuanzia Sh15 hadi Sh500 na kuwataka kusaini karatasi inayoonyesha wamepokea kiasi hicho.
Wakati mwingine, amesema walilazimishwa kusaini mikataba mipya yenye masharti ambayo hayajadiliwa kikamilifu.
Kutokana na hali hiyo, amesema baadhi ya wafanyakazi waliamua kuungana kudai malipo ya miezi minne wanayodai ambayo hawakulipwa.
Amesema wanatarajia mamlaka husika zitaangalia malalamiko yao ili kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa kulingana na sheria za kazi katika mradihuo mkubwa wa kimkakati.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Silinde Gumada amesema ili kumaliza mgogoro huo wameita uongozi wa kampuni hiyo, ambayo iliwakilishwa na wakili wake pamoja na ofisa mwajiri.
“Baada ya kusikiliza walalamikaji tuliandika barua ya wito kwa mwajiri na walikuja hapa kusikiliza madai ya wafanyakazi na wao, walisema wanakwenda kukaa na menejimenti ili kupata majibu,” amesema Gumada.
Amesema wafanyakazi hao wamewasilisha malalamiko mengi ikiwepo maripo ya notisi ya siku 28 kabla ya kufutwa kazi, kulipwa mishahara ya siku zote walizofanya kazi, pamoja na mishahara ya likizo ambazo hawajatumia.
Amesema wapo wafanyakazi ambao walitakiwa kuachishwa kazi baada ya kuonekana meadi unafikia tamati, hivyo kupata haki zao wamekuwa na malalamiko ambayo walifikisha maeneo mbalimbali na mwisho kuyapeleka katika klini ya sheria baada ya kukosa muafaka wa jambo lao.
Aidha, wafanyakazi hao wanadai malipo ya kinuwa mgongo kwa wale ambao wanapunguzwa kazi ambapo kimsingi kwa kila mwaka wa huduma, mfanyakazi anastahili kulipwa siku saba kulingana na mshahara wake wa msingi.
Malipo haya yanaongeza pamoja na posho za gharama za usafiri na gharama pale wanapofutwa ajira au kuondolewa kazini.
Amesema wafanyakazi pia wamelalamika kuhusu malipo ya muda wa ziada, ambapo kwa mujibu wa sheria, mfanyakazi anapofanya kazi zaidi ya masaa yaliyokubaliwa kwa siku au wiki, mwajiri anapaswa kulipwa posho ya ziada hivyo baadhi ya wafanyakazi wa ndani hawapati huduma bora kama wenzake wa kigeni, ikiwemo chakula, malazi, na usafiri, hali inayosababisha changamoto kubwa kwa wafanyakazi wa ndani.
“Kimsingi kila mfanyakazi anapaswa kuheshimiwa kwa mujibu wa sheria. Ikiwa hakuna mgogoro, hakuna haja ya kupeleka hoja mahakamani. Lakini pale ambapo haki zao hazitimizwi, pale ndipo hoja za kisheria zinapopaswa kushughulikiwa,” amesema
Amesema wafanyakazi wa kigeni hupatiwa huduma bora zaidi, ikiwemo chakula na usafiri unaowafikisha hadi wanakoishi, wakati wafanyakazi wa ndani hulazimika kushuka mbali na makazi yao na kujitafutia usafiri kama bodaboda.
“Wenzetu wanafikishwa hadi mlangoni wanakoishi, lakini sisi tunashushwa njiani na kujitafutia usafiri kwa gharama zetu.”
Malalamiko mengine yanahusu malipo wanayopata wanapofanya kazi baharini, wakidai kuwa kazi hiyo ni hatarishi lakini malipo wanayopata ni madogo.
“Mtu mwingine akienda kufanya kazi kama hiyo analipwa zaidi ya Sh100,000 kwa siku, lakini sisi tunapewa takribani Sh1000 tu,” alidai mfanyakazi mmoja.
Aidha, amedai mfumo wa bima ya afya waliyopewa baadhi ya wafanyakazi haukidhi mahitaji yao, hivyo wakati mwingine hulazimika kuchangia fedha zao ili kugharamia matibabu wanapougua au kujeruhiwa kazini.
Pia, amesema wamekuwa wakizunguka katika ofisi za mkuu wa mkoa ili kupata muafaka wa jambo lao lakini imekuwa ni shida na mara ya mwisho kukutana na mkuu huyo ni Jumatatu ya Machi 2, 2026 ambayo aliwataka kuwa wavumilivu kusubiri kliniki ya sheria.
Amesema wamekuwa wakigoma mara kadhaa na kukatwa malipo yao kutokana na migomo waliyofanya jambo ambalo limekuwa likiwaumiza kwani wamekuwa wakifai haki zao za msingi.
“Tunaona wenzetu wanalipwa vizuri na chakula kizuri lakini sisi imefikia hatua tunakula chakula kibovu na mlo mara moja wakati wenzetu wanalipwa Sh 8000 kwa ajili ya chakula kwa siku,”amesema.
Aidha, Andasoni amesema masuala mengine ni pamoja na muda wa kazi unaofanywa kila siku na kwa wiki. Wafanyakazi wanajikuta wakiendesha kazi kwa saa zaidi ya zilizopangwa, mara nyingine bila malipo ya muda wa ziada (overtime).
Pia, kufanya kazi siku za Jumamosi bila malipo yanayostahili kimekuwa tatizo linalozua malalamiko.
“Wafanyakazi wa ndani wanashughulika na hatari kubwa, lakini baadhi ya stahiki na haki zinazostahili kulipwa hazitolewa. Hali hii inapelekea kutoeleweka na kutozingatia uwiano wa haki kazini,” alisema Andasoni.
Wafanyakazi hao wanasema walifika Kliniki ya Sheria kueleza changamoto hizi kwa mawakili wa Serikali, wakitarajia kupata mwongozo wa kisheria kuhusu hatua za kuchukua ili kudai haki zao kulingana na sheria za kazi.
Kwa mujibu wa Andasoni, wafanyakazi hao pia wamekuwa wakilalamikia mikataba ya ajira ambayo wamekuwa wakigoma mara kwa mara tangu 2023 na kuongezewa kiasi cha pesa kuanzia Sh15 hadi Sh500 na kuwataka kusaini karatasi inayoonyesha wamepokea kiasi hicho na wakati mwingine hulazimishwa kusaini mikataba mipya yenye masharti ambayo hayajadiliwa kikamilifu.
Kutokana na hali hiyo, amesema baadhi ya wafanyakazi waliamua kuungana kudai malipo ya miezi minne wanayodai yanahusiana na stahiki mbalimbali ambazo hawakulipwa.
Andasoni amesema wanatarajia mamlaka husika kuangalia malalamiko yao ili kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa kulingana na sheria za kazi, hasa ikizingatiwa kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati katika sekta ya nishati.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Silinde Gumada amesema kumaliza mgogoro huo wameita kampuni hiyo ambayo iliwakilishwa na wakili wao pamoja na Ofisa mwajiri na makubaliano wanapeleka barua iliyoandikwa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali kwa menejimenti.
“Baada ya kusikiliza walalamikaji tuliandika barua ya wito kwa mwajiri na walikuja hapa kusikiliza madai ya wafanyakazi na wao walisema wanakwenda kukaa na menejimenti ili kupata majibu ya maombi yaliyotolewa,” amesema Gumada.