Global Publishers
March 12, 2026
0 Comments
Israel Defense Forces imesema iko tayari kuendelea na vita dhidi ya Iran kwa muda mrefu kadri itakavyohitajika hadi malengo ya kijeshi yatakapofikiwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na Reuters, msemaji wa jeshi la Israel Avichay Adraee alisema kuwa Israel itaendelea kujibu mashambulizi baada ya kundi la Hezbollah kuanzisha kile alichokiita operesheni mpya.
Jeshi la Israel pia limedai kufanya wimbi kubwa la mashambulizi katika maeneo ya Beirut nchini Lebanon jioni ya leo.
Wakati huo huo, Israel Katz, Waziri wa Ulinzi wa Israel, amesema kuwa mapigano hayo yanaweza kuendelea bila kikomo cha muda.
Amesisitiza kuwa operesheni hiyo itaendelea hadi malengo yote ya ushirikiano wa kijeshi kati ya Israel na Marekani yatakapokamilika.
Kauli hiyo inaonyesha kuwa viongozi wa Israel wanaona uwezekano wa vita hiyo kuendelea kwa muda mrefu, huku mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati ukiendelea kuongezeka.