Rais Samia Akutana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Afrika

Global Publishers
March 11, 2026
0 Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika (UNOAU) Bw. Parfait Onanga-Anyanga, tarehe 11 Machi, 2026 Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amekutana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika (UNOAU), Parfait Onanga-Anyanga, tarehe 11 Machi 2026, Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Kikao hicho kililenga kujadili masuala ya ushirikiano wa kidiplomasia, amani na maendeleo ya bara la Afrika, huku pande zote zikisisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kuleta maendeleo endelevu na utulivu katika eneo la kieneo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sukari ya ABF ya Uingereza Bw. Paul Kenward, tarehe 11 Machi, 2026 Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sukari ya ABF ya Uingereza Bw. Paul Kenward, tarehe 11 Machi, 2026 Ikulu ya Chamwino, Dodoma.