Global Publishers
March 13, 2026
0 Comments
Diwani wa Kata ya Kariakoo, Haji Manara, amezungumzia kuhusu marehemu Denis Busulwa almaarufu Ssebo, akimwelezea kama mtu aliyekuwa na moyo mkubwa wa kusaidia watu na aliyependa kuwa karibu na jamii enzi za uhai wake.
Manara amesema Ssebo alikuwa mtu mwenye upendo na mshikamano mkubwa, ambaye alijenga urafiki na watu wengi ndani na nje ya tasnia ya habari. Ameongeza kuwa mchango wake katika vyombo vya habari nchini, hususan katika uongozi wa EFM na TVE, utaendelea kukumbukwa kwa muda mrefu.
Aidha, Manara ameeleza kuwa kifo cha Ssebo ni pigo kubwa si tu kwa familia yake, bali pia kwa marafiki, wafanyakazi wenzake na wadau wa tasnia ya habari nchini.