WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 13, 2026 ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Kata ya Shanwe, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 22.8 umefikia asilimia 55 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika Julai 2026. Kukamilika kwake kutasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa eneo hilo.
Baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Dkt. Mwigulu amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa ili wananchi waanze kunufaika na huduma ya maji.
Mradi huo unatarajiwa kuzalisha takribani lita milioni 12 za maji kwa siku.






