Video: Mtumbwi Wapinduka na Kuua Watumishi 6, Miili 3 Haijapatikana Kigoma

Bakari Mahundu
March 13, 2026
0 Comments

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amrmetoa pole kwa uongozi wa Wilaya ya Kigoma mkoani hapa kufuatia tukio la vifo vya watumishi  sita wa Idara ya Afya waliofariki dunia kufuatia chombo walichokuwa wakisafiria kukumbwa na dhoruba kisha kuzama katika Ziwa Tanganyika asubuhi ya leo Machi 13, 2026 katika kijiji cha Kalalangabo wilayani humo.

Balozi  Sirro amesema waliofariki ni miongoni mwa watendaji 18 walikuwa wakisafiri kwa kutumia chombo hicho kuelekea katika kijiji cha Kagunga wilayani humo kwa ajili ya kuendesha zoezi la chanjo na usajili wa bima ya Afya kwa wote.

Amesema kati ya waliofariki, miili sita imepatikana huku  wengine watatu wakiendelea kutafutwa kwa ushirikiano wa vyombo vya usalama na wananchi, huku akitoa tahadhari kwa watumiaji na wasafiri kupitia ziwa hilo kuzingatia tahadhari zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini.