Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema wananchi wa Marekani kujua kwamba utawala haramu wa Israel umeiburuta Marekani na kuitumbukiza kwenye vita na Iran.
Ismail Baqaei amesema hayo aliporusha hewani tena ujumbe wa seneta wa Marekani, Chris Murphy kwenye mtandao wa kijamii wa X uliosema: Hili ndilo jambo ambalo watu wa zamani kulijua.
Baada ya kikao katika kikao cha viongozi wa serikali ya Donald Trump kuhusu vita vya sasa dhidi ya Iran, Seneta wa chama cha Domocratic, Chris Murphy, amekosoa mwelekeo wa sasa wa serikali ya Washington na kusema: Israel imetulazimisha jambo hili, na suala hili linaonesha udhaifu mkubwa wa Marekani kwamba waitifaki wetu tunaweza kuibua mambo muhimu kwa maslahi ya taifa letu. “Tumekuwa dhaifu kiasi gani?” amesema Seneta Chris Murphy.