Global Publishers
March 13, 2026
0 Comments
Jiji la Dubai limeanza kuonekana kama mji uliotelekezwa baada ya maelfu ya wakazi na wageni kuondoka kufuatia mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani yanayodaiwa kutoka Iran.
Ripoti zinaeleza kuwa maeneo maarufu ya mapumziko kama Jumeirah Beach na hoteli za kifahari kwenye Palm Jumeirah yamebaki tupu, huku viti vya jua, mabwawa ya kuogelea na fukwe ambazo kawaida hujaa watalii sasa zikiwa hazina watu.

Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani pia yanaripotiwa kusababisha uharibifu katika baadhi ya majengo ya wilaya ya kifedha ya Dubai, huku hoteli maarufu ya Fairmont The Palm ikitajwa kuguswa na mashambulizi hayo.
Dubai kwa muda mrefu imekuwa kivutio kikubwa kwa wageni kutoka United Kingdom na mataifa mengine, ikiwa na zaidi ya Waingereza 240,000 wanaoishi au kutembelea mara kwa mara. Hata hivyo, kutokana na hali ya vita, maelfu wameripotiwa kuondoka huku safari za ndege kutoka jiji hilo zikiongezeka bei kwa kasi.
