KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UJENZI WA KAMPASI YA CHUO KIKUU MZUMBE GOMBERO MKINGA MKOANI TANGA

*******

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu Utamaduni na Michezo imeridhishwa na uwepo wa mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe Gombero Wilayani Mkinga Mkoani Tanga.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara katika eneo hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko ameipongeza Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maamuzi ya kuleta fedha za kujenga kampasi ya Mzumbe Mkoani Tanga na kwamba wmeahidi  kuendelea kushirikiana Wizara kuhakikisha chuo hicho kinaletewa huduma za kijamii ili kuwezesha shughuli za kielimu kuanza kwa ufanisi.

Amesema ziara hiyo ni utaratibu wa kikakuni wa Bunge ambapo kwa sasa wanaangalia utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2025/2026  kwamba Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.

 “Sisi kama Kamati tumepita kukagua kwa yale ambayo tumekasimiwa kuyafanya, niwaombe muendelee kutekeleza mradi huu vizuri ili hata kwa maeneo yale ya wengine wakipita  watoke na maneno hayahaya asione dosari yoyote katika matimizi ya fedha au mifumo  mingine,” amesema Mhe. Sekiboko

Na kuongeza “Tumefurahishwa kuona ilani ya Chama cha Mapinduzi imetekelezwa vizuri katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,”

Mhe. Sekiboko ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau mbalimbali kuja kuwekeza Mkoa wa Tanga hususan katika maeneo yaliyozunguka Chuo  hicho huku akimpongeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Mkenda na Menejimenti kwa kuhakisha Mradi huu umetekelezwa Mkoani Tanga na kwa ufanisi.