Bi.Fauzia Malik na Bi.Angelic wateuliwa Bodi ya Wakurugenzi Equity Bank Tanzania

Equity Bank Tanzania imewateua Bi. Malik na Bi. Tarimo kwenye Bodi ya wakurugenzi na inatarajia kufaidika na ujuzi wao mkubwa huku Benki ikiendelea kuimarisha jukumu lake katika kukuza ushirikishwaji wa kifedha, kusaidia biashara ndogo na za kati, na kuleta ukuaji endelevu wa kiuchumi Tanzania.

Akizungumzia uteuzi huo, Dkt. Florens Martin Turuka, Mwenyekiti wa Equity Bank Tanzania, alisema: “Tunafuraha kuwakaribisha Fauzia Malik na Angelica Tarimo kwenye Bodi ya Equity Bank Tanzania. Uzoefu wao mkubwa katika ujasiriamali, utawala bora, na uongozi wa kimkakati utaongeza thamani kubwa kwenye Bodi tunapoendelea kuongoza ukuaji na mageuzi ya Benki yetu.”

Kwa uteuzi huu, Bodi sasa ina jumla ya wanawake watano kati ya wakurugenzi, ikiangazia uongozi wa Equity Bank Tanzania katika kuendeleza usawa wa kijinsia na utawala jumuishi katika sekta ya huduma za kifedha nchini Tanzania.