Kihongosi Ampongeza Mbunge Shigongo Kwa Utendaji Mzuri Buchosa – Video

Global Publishers
March 14, 2026
0 Comments

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amempongeza Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, kwa utendaji wake mzuri na juhudi anazozifanya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

Kihongosi ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake katika Jimbo la Buchosa, akisema kuwa Shigongo ameonesha uongozi wa kweli na kujitoa kwa dhati katika kusimamia maendeleo pamoja na kupambania maslahi ya wananchi.

Amesema kazi zinazofanywa na mbunge huyo zinaonekana wazi kwa wananchi na zinaakisi dhamira ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuwaletea Watanzania maendeleo.