Global Publishers
March 14, 2026
0 Comments
Mkurugenzi wa Vipindi wa EFM Tanzania, Dickson Ponela maarufu kama Big Daddy Dizzo, leo Machi 14, 2026 alitoa taarifa ya mabadiliko ya eneo la tukio la kumuaga kwa heshima aliyekuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Biashara wa EFM Tanzania na TVE Tanzania, marehemu Dennis Busulwa maarufu kama Ssebo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, badala ya tukio hilo kufanyika katika Viwanja vya Posta (TTCL Grounds) Kijitonyama, sasa shughuli hiyo inafanyika katika Parokia ya Mtakatifu Martha Mikocheni B jijini Dar es Salaam.
Mabadiliko hayo yamefanywa kutokana na hali mbaya ya hewa iliyojitokeza. Misa ya kumuaga marehemu itaanza saa sita mchana katika kanisa hilo.