Global Publishers
March 14, 2026
0 Comments
Msanii mwenye hekaheka zake mjini asiyeishiwa vibwanga Gift Stanford ‘Gigy Money’ ambaye kwa sasa amebadili dini na kutumia jina la Rawya, amefunga ndoa na mpenzi wake Licky katika sherehe iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Ndoa hiyo ilifungwa na kuambatana na sherehe fupi iliyofanyika katika Viwanja vya Lugalo Golf Club, ambapo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wasanii na watu maarufu kama Shilole, Hamisa Mobetto, Queen Darling na Jay Melody pamoja na wachekeshaji na wageni wengine waalikwa.
Akizungumza katika sherehe hiyo, Rawya (Gigy Money) ameahidi kumtunza mumewe Tarick, akisisitiza kuwa hayuko tayari kuona ndoa ya pili wala hataki ndoa yake hiyo kuvunjika.

