Mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya Simba dhidi ya TRA United umeahirishwa kutokana na miundombinu ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kujaa maji kutona na mvua zinazonyesha maeneo mbalimbali ya nchi.
 Akizungumza na Azam TV, Kamishna wa mchezo huo Mussa Nyamandege amethibitisha kuhairishwa kwa mchezo huo wa ligi baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maji kujaa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid na hivyo kufanya mpira kushindwa kutembea uwanjani.
Ameongeza kuwa, mchezo huo uliokuwa umepangwa kuanza saa 10:00 jioni leo utapangiwa siku nyingine na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).