Global Publishers
March 14, 2026
0 Comments
Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho leo Machi 14, 2026 amesema kuwa kifo ni fumbo na kila mwanadamu anapaswa kujiandaa nacho kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kukikwepa.
Mrisho ameyasema hayo kufuatia kumalizika kwa ibada ya kumuombea aliyekuwa mfanyabiashara maarufu Ssebo, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Martha Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya ibada hiyo, Mrisho amesema tukio la kifo linapaswa kuwa funzo kwa kila mtu kutambua kuwa maisha ya mwanadamu yana kikomo, hivyo ni muhimu kuishi kwa kufuata maadili mema na kumcha Mungu.
Amesisitiza kuwa njia bora ya kujiandaa na kifo ni kuzingatia mafundisho yaliyopo katika vitabu vitakatifu kwa kufanya yale yaliyoamrishwa na kuepuka mambo yote yaliyokatazwa.
Amesema kuwa kufanya mema na kuishi kwa haki kunasaidia mtu kuwa tayari wakati wowote anapokabiliwa na safari ya mwisho ya maisha.