Global Publishers
March 14, 2026
0 Comments
MECHI ya TRA United vs Simba iliyotarajiwa kuchezwa leo Machi 14,2026 imeahirishwa kutokana na Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kujaa maji.
Kwa mujibu wa Kamishna wa mchezo kati ya TRA United vs Simba SC mechi namba namba 7, Mussa Nyamandege amebainisha kuwa pande zote mbili zimeridhia maamuzi hayo.
“Kutokana na sheria namba 1 kutokubalika kwa kuwa mpira haudundi hivyo mchezo huu kati ya TRA United vs Simba SC utapangiwa tarehe nyingine na bodi, timu zote mbili zimeridhia,”.
Tayari timu zote mbili ziliwasili uwanjani kwa ajili ya mchezo huo wa NBC Premier League uliotarajiwa kuanza saa 10:00 jioni kwa wababe hao kusaka pointi tatu muhimu.
Timu zote pia zilitambulisha vikosi kazi kwa ajili ya mchezo huo ambao sasa utapangiwa tarehe nyingine na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB).
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.