STANDARD CHARTERED TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA MCHANGO NA ELIMU YA FEDHA KATIKA HOSPITALI YA CCBRT

Dar es Salaam, Tanzania – 13 Machi 2026 – Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Standard Chartered Tanzania imetembelea Hospitali ya CCBRT na kutoa mashine 12 za kushona kwa ajili yakuunga mkono Mpango wa Mabinti, unaolenga kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitiamafunzo ya ujuzi na programu za urekebishaji wa maisha.

Mashine hizo zitatumika katika Kituo cha Mabinti kusaidia wanufaika kujifunza ujuzi wa ushonaji kwavitendo, ili waweze kujipatia kipato na kujenga maisha ya kujitegemea na endelevu. Mchango huo nisehemu ya jitihada za Standard Chartered kuunga mkono mipango ya kijamii inayochochea uwezeshajiwa wanawake na ushirikishwaji wa kiuchumi.

Wakati wa ziara hiyo, wafanyakazi wa Standard Chartered Tanzania pia waliendesha kikao cha elimu yafedha kwa wanufaika wa Kituo cha Mabinti. Mafunzo hayo yalilenga kuwapatia washiriki maarifa yamsingi kuhusu usimamizi wa fedha binafsi, ikiwa ni pamoja na kupanga bajeti, kuweka akiba na kupangamustakabali wa kujitegemea kifedha.

Kama sehemu ya shughuli za siku hiyo, timu ya benki ilitembelea pia wodi ya wagonjwa wa fistula katikaHospitali ya CCBRT, ambapo walipata fursa ya kutumia muda na wagonjwa pamoja na kugawa vifurushivya mahitaji kwa wanawake wanaopokea matibabu. Ziara hiyo ililenga kutoa faraja na kuhamasishawagonjwa wanaoendelea na matibabu na kupona.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Desideria Mwegelo – Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Taasisi, Chapa na Masoko Tanzania na Mkuu wa Masoko ya CIB Afrika alisisitiza dhamira ya benki katika kukuzamaendeleo jumuishi kwa kuunga mkono mipango inayowawezesha wanawake na wasichana katika jamii.

Ushirikiano wa Standard Chartered na CCBRT unaakisi dhamira pana ya benki ya kuchochea biasharana ustawi wa jamii kupitia ushiriki wa kijamii, hususan kwa kuunga mkono programu zinazowapatiawanawake ujuzi, heshima na fursa za maisha bora ya baadaye.