MKUTANO WA MAALUM (KIKAO CHA 3) WA BUNGE LA TANO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EALA) TAREHE 16 MACHI 2026

******

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) kuwa Mbunge katika Bunge hilo leo tarehe 16 Machi 2026 katika mkutano Maalum wa Bunge la Tano la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya Mtandao (virtual platform).

Mhe. Waziri Waziri Kombo, ameapa kuwa` Mbunge kwa wadhifa wake wa uwaziri (ex-officio) kwa mujibu wa mujibu wa Kanuni ya 5 (4) ya Kanuni za Bunge la Afrika Mashariki ambayo inabainisha kuwa “mbunge hataweza kuketi bungeni bila kula kiapo cha utii wa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki”.