*****
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua huduma mpya ya intaneti ya kasi kubwa ijulikanayo Faiba Supersonic Experience, Kasi Balaa kwa lengo la kuimarisha huduma za mawasiliano nchini.
Uzinduzi huo ni sehemu ya juhudi za TTCL kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya kidijitali na mahitaji ya watumiaji wa intaneti.
Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL, Vedastus Mwita amesema huduma hiyo imeboreshwa ili kusaidia matumizi mbalimbali ya teknolojia katika maisha ya kila siku.
Amesema huduma hiyo itasaidia matumizi kama Smart Home, Smart Office, biashara mtandaoni pamoja na michezo na burudani za mtandaoni.
Mwita amesema TTCL imeboresha vifurushi vya intaneti ili kuwapa wateja kasi kubwa na huduma yenye uhakika zaidi.
Amevitaja vifurushi hivyo kuwa ni T-Fiber Busta chenye kasi ya 60/60 Mbps kwa gharama ya Sh55,000 kwa mwezi pamoja na dakika 250 za simu ya mezani.
Vifurushi vingine ni T-Fiber Triple Hub Plus chenye kasi ya 100/100 Mbps kwa Sh70,000 kwa mwezi na Triple Hub Extra chenye kasi ya 150/150 Mbps kwa Sh100,000 kwa mwezi.
Aidha kuna Triple Hub Balaa chenye kasi ya 200/200 Mbps kwa Sh150,000 kwa mwezi pamoja na Triple Hub Jumbo chenye kasi ya 250/250 Mbps kwa Sh200,000 kwa mwezi.
.webp)


.webp)
