……………
Na Saidi Lufune, Katavi
Wakati Tanzania ikijiandaa kuadhimisha siku ya misitu Duniani Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amewataka watanzania kushirikiana na Taasisi za uhifadhi nchini katika uhifadhi wa Misitu kuongeza chachu ya maendeleo endelevu kupitia misitu iliyopo hapa nchini
Mhe. Chande amebainisha hayo Mkoani Katavi katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), katika maeneo mbalimbali hapa nchini
”Endeleeni kushirikiana na Taasisi zetu za uhifadhi, Ili kusudi tubaki na maendeleo endelevu hasahasa katika maswala ya kilimo, kwa sababu bila ya misitu hakuna chakula, bila mvua hakuna chakula kwa hiyo ni muhimu sana kuhifadhi Misitu yetu kwa kushirikiana” amesisitiza Mhe. Chande
Akizungumza juu ya swala la uhifadhi wa Misitu ya jamii na manufaa yake, Mhe. Chande ameahidi kuwa wizara itaendelea kushirikiana kwa karibu na jamii na viongozi kubainisha mipaka ya maeneo ya hifadhi za Misitu na misitu ya jamii ili kuishi kwa mapenzi na utu kati ya Wizara, taasisi na wananchi






