Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Maendeleo (TIB), Deogratius Kwiyukwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Shigeki Komatsubara wakisaini hati ya Makubaliano (MoU) itakayolenga kuendeleza mifumo bunifu ya ufadhili wa maendeleo, hatua inayotarajiwa kuchochea mageuzi ya kijamii na kiuchumi nchini. Mikataba huo umesainiwa leo Machi 17, 2026 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Maendeleo (TIB), Deogratius Kwiyukwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Shigeki Komatsubara wakibadilishana hati ya Makubaliano (MoU) itakayolenga kuendeleza mifumo bunifu ya ufadhili wa maendeleo, hatua inayotarajiwa kuchochea mageuzi ya kijamii na kiuchumi nchini. Mikataba huo umesainiwa leo Machi 17, 2026 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Maendeleo (TIB), Deogratius Kwiyukwa akizungumza leo Machi 17, 2026 wakati wa kusaini hati ya Makubaliano (MoU) itakayolenga kuendeleza mifumo bunifu ya ufadhili wa maendeleo, hatua inayotarajiwa kuchochea mageuzi ya kijamii na kiuchumi nchini. Mikataba huo umesainiwa leo Machi 17, 2026 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Shigeki Komatsubara akizungumza leo Machi 17, 2026 wakati wa kusaini hati ya Makubaliano (MoU) itakayolenga kuendeleza mifumo bunifu ya ufadhili wa maendeleo, hatua inayotarajiwa kuchochea mageuzi ya kijamii na kiuchumi nchini. Mikataba huo umesainiwa leo Machi 17, 2026 jijini Dar es Salaam.
Na Avila Kakingoi, Michuzi Tv
BENKI ya Maendeleo TIB kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wamesaini Hati ya Makubaliano (MoU) itakayolenga kuendeleza mifumo bunifu ya ufadhili wa maendeleo, hatua inayotarajiwa kuchochea mageuzi ya kijamii na kiuchumi nchini.
Makubaliano hayo yaliyosainiwa jijini Dar es Salaam leo Machi 17, 2026 yatafungua fursa mpya za kuibua na kuendeleza miradi bunifu yenye tija na uwezo wa kuvutia uwekezaji, sambamba na vipaumbele vya taifa.
Sekta zitakazonufaika ni pamoja na nishati jadidifu, maendeleo ya biashara ndogo na za kati (SMEs), uchumi wa buluu pamoja na miradi inayoongozwa na vijana.
Kupitia ushirikiano huo, taasisi hizo mbili zitashirikiana kutambua na kuandaa miradi ya kimkakati itakayoongeza utayari wa uwekezaji, kuhamasisha matumizi ya mifumo ya ufadhili mseto (blended finance) na kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi.
Aidha, makubaliano hayo yanatarajiwa kuimarisha uwezo wa taasisi, kukuza ujasiriamali na kupanua fursa za kiuchumi kwa jamii.
Akizungumza wakati wa kusaini mikata hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Deogratius Kwiyukwa amesema ushirikiano huo unaakisi dhamira ya pamoja ya kuharakisha maendeleo endelevu nchini kwa kuunganisha mitaji ya muda mrefu na suluhisho bunifu za kifedha.
“Ushirikiano huu utachochea uwekezaji wenye mageuzi katika sekta muhimu za uchumi wetu, na kuiwezesha TIB kuendelea kutekeleza wajibu wake wa kusaidia miradi ya maendeleo yenye tija kwa taifa,” amesema.
Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Shigeki Komatsubara amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za maendeleo na taasisi za kifedha za ndani katika kuongeza athari za maendeleo.
Amesema kupitia makubaliano hayo, UNDP inalenga kufungua mifumo mipya ya ufadhili itakayochochea ukuaji jumuishi, kuimarisha ustahimilivu wa uchumi na kupanua fursa za maendeleo kwa Watanzania.
Ushirikiano huo unaendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na juhudi za serikali chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan za kuharakisha mageuzi ya kiuchumi, kuimarisha uwekezaji na kulinda rasilimali za mazingira.
Hati hiyo ya makubaliano imeweka msingi wa utekelezaji wa miradi ya pamoja, ushirikiano wa kitaalamu na uhamasishaji wa rasilimali, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuunda ajira, hususan kwa vijana, na kujenga uchumi endelevu na shindani nchini.

.jpeg)

