Global Publishers
March 18, 2026
0 Comments
Tukio lililozua taharuki kubwa wiki iliyopita katika eneo la Mtoni Mtongani, mtaa wa Nuru, limeibua maswali mazito ya kisheria na kijamii baada ya Athumani Musa kudaiwa kuuza nyumba ya familia bila kumshirikisha mke wake, Neema.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Athumani anadaiwa kufanya uamuzi wa kuuza nyumba hiyo bila ridhaa ya mke wake, hali iliyosababisha mgogoro mkubwa wa kifamilia.
Inadaiwa kuwa baada ya kukamilisha mauzo hayo, alichukua hatua ya kuwatuma watu waliodaiwa kuwa na nguvu ili kuwatoa kwa lazima mke wake pamoja na mtoto wao kutoka ndani ya nyumba hiyo.
Kupitia Global TV, Athumani amefunguka na kueleza kuwa alinunua nyumba hiyo mara baada ya kuachana na mke wake.