Seneta wa Marekani: Trump ni mpumbavu/ Panetta: Utawala wa Iran umekita mizizi, ni imara

Seneta wa chama cha Democratic cha Marekani amemtaja rais wa nchi hiyo kuwa mjinga kwa kufuata kibubusa sera za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Akikosoa sera za kutafuta vita vya utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Seneta wa chama cha Democratic, Chris Holen, amwemwita mpumbavu kwa maagizo ya Tel Aviv.

Akizungumzia majadiliano ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Israel dhidi ya Iran, Holen amesema: “Vita hivi vinaifanya Marekani na kufikia kutokuwa na usalama zaidi.

“Tumefungua sanduku la Pandora. Wanajeshi wote wa Marekani wameuawa na raia nchini Iran, wakiwemo watoto wa shule ya kike, wameshambuliwa. Amesema maabilioni ya dola yamepotea katika vita hivi.

Wakati huo huo, Waziri wa zamani wa Vita wa Marekani amesema: Vita dhidi ya Iran vilianza na hoja kwamba tunaingia vitani ili tuweze kubadilisha serikali nchini Iran na kuwalazimisha watu wa Iran kuipindua serikali. Matokeo yake ni kwamba, serikali ya Iran haitabadilika, wao ndio watakaokuwa washindi wa vita hivi.

Sambamba na upinzani nchini ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran, Waziri wa zamani wa Vita wa Marekani, Leon Panetta amesema: “Tunachokiona Iran ni kwamba serikali imeimarika zaidi, na kwa kuchaguliwa kiongozi mpya, sasa wanahisi wana nguvu zaidi.”

Leon Panetta

Panetta amesisitiza: “Hisia hii ya kuwa na nguvu pia inatokana na uwezo wao wa kuiwekea Marekani mashinikizo.” Amekiri kwamba: “Utawala wa Iran umekita mizizi zaidi na uko imara kuliko tulivyofikiria.”