-NI KATIKA SHULE ZA MSINGI SIMA A NA MADARAKA, IKITIMIZA ILIYOTOLEWA WAKATI WA MSAFARA WA TWENDE BUTIAMA 2025.
Simiyu & Mara, Tanzania 17Machi 2026: Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na wadau wake wakiwemo Stanbic Bank Tanzania pamoja na waandaaji wa msafara wa Twende Butiama, wamekabidhi rasmi miundombinu ya vyoo katika Shule za Msingi Sima A iliyopo Bariadi mkoani Simiyu pamoja na Shule ya Msingi Madaraka iliyopo Butiama mkoani Mara.
Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa wakati wa msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama uliofanyika Julai mwaka jana, uliolenga kumuenzi Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere huku ukihamasisha maendeleo ya jamii hususan katika sekta za elimu, afya na mazingira.
Kupitia mradi huo, jumla ya matundu ya kisasa ya vyoo 20, kumi kila shule yamejengwa katika shule hizo, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi pamoja na kusaidia kulinda afya na ustawi wao shuleni.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa wa Vodacom Tanzania Plc Ezekiel Nungwi alisema kampuni hiyo inaendelea kushirikiana na jamii katika kuboresha mazingira ya elimu nchini.
“Kupitia taasisi yetu ya Vodacom Tanzania Foundation tunaamini kuwa uwekezaji katika elimu ni uwekezaji katika mustakabali wa taifa. Ujenzi wa miundombinu hii ya vyoo ni sehemu ya kutimiza ahadi tuliyoitoa wakati wa msafara wa Twende Butiama uliofanyika mwaka jana na pia mchango wetu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira salama na bora ya kujifunzia,” alisema Bw Nungwi.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sima A XXX aliishukuru Vodacom Tanzania pamoja na wadau wake kwa msaada huo, akieleza kuwa mradi huu utasaidia kuboresha hali ya usafi na afya ya wanafunzi shuleni huku ikiongeza ufaulu wao darasani.
“Ujenzi wa vyoo hivi ni msaada mkubwa kwa shule yetu. Miundombinu hii itasaidia kupunguza changamoto tuliyokuwa nayo ya uhaba wa vyoo na kuwapa wanafunzi mazingira bora na salama ya kujifunzia,” alisema.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Madaraka XXX iliyopo wilayani Butiama alisema mradi huo utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha mazingira ya shule na ustawi wa wanafunzi.
“Tunawashukuru sana Vodacom Tanzania Foundation na wadau wao kwa kutukumbuka. Miundombinu hii itasaidia kuboresha usafi wa mazingira ya shule na kuwafanya wanafunzi wawe na muda mwingi zaidi wa kujifunza badala ya kupoteza muda kusubiri huduma ya choo,” alisema.
Mbali na kuboresha miundombinu ya shule, mradi huo pia unalenga kuhamasisha wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla kuzingatia matumizi ya vyoo bora na kuendeleza usafi wa mazingira.
Kupitia miradi yake ya kijamii, Vodacom Tanzania Foundation inaendelea kuwekeza katika maeneo muhimu ya maendeleo ya jamii ikiwemo elimu, afya na mazingira, kwa lengo la kuchangia ustawi wa Watanzania na maendeleo endelevu ya jamii.
Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania PLC, Ezekiel Nungwi (wa tatu kushoto)na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Madaraka Deocray Mtayomba (wa tatu kulia)wakikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua vyoo vipya na vya kisasa kumi vilivyojengwa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation katika shule ya msingi Madaraka iliyopo Butiama Mkoani Mara. Baadhi ya vyoo hivyo vimezingatia pia uhitaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu na vimetolewa ili kutimiza dhamira ya Vodacom Foundation Tanzania ya kuchangia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wote, huku ikiangazia afya na ustawi wa wanafunzi kupitia miradi ya Maendeleo ya jamii. Tukio hilo limefayika jumatatu wiki hii na kuhudhuriwa na wajumbe wa kamati ya shule, wazazi, walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Madaraka iliyoko wilayani Butiama Deocray Mtayomba (kushoto) akielezea kuhusu ubora wa vyoo vipya kwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania Plc, Ezekiel Nungwi, baada ya uzinduzi wa choo cha kisasa chenye matundu kumi kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Madaraka iliyopo mkoani Mara.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Madaraka iliyopo Kiabakari wilayani Butiama mkoani Mara wakati wa hafla ya kukabidhi vyoo vya kisasa vyenye matundu kumi ambapo baadhi ya vyoo hivyo vimezingatia mahitaji wanafunzi wenye mahitaji maalumu

