Global Publishers
March 19, 2026
0 Comments
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir Bin Ally, Sikukuu ya Eid El-Fitri itafanyika siku ya Jumamosi, Machi 21, 2026.
Amesema kuwa mwezi hauonekani (haujakandama) siku ya Machi 19, 2026 ambayo ni sawa na Ramadhani ya 29. Hivyo, mfungo utaendelea na siku ya Alhamisi Machi 20 itakuwa ni Ramadhani ya 30, na hatimaye Eid El-Fitri itaswaliwa Jumamosi Machi 21.
Taarifa hiyo inahitimisha ratiba ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa mwaka huu nchini Tanzania.