Global Publishers
March 20, 2026
0 Comments
Mdogo wa marehemu, Athumani Nyanza, pamoja na Hawa Nyanza, wamezungumza kwa uchungu baada ya kueleza tukio la kushangaza walilolipata walipofika katika eneo ambalo lilidaiwa kuwa ndiko ndugu yao alikozikwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya familia, baada ya kufika eneo hilo na kufanya uchunguzi wa kina, walifukua kaburi hilo na kukuta mwili uliodaiwa kuwa wa ndugu yao ukiwa tayari umeshafariki dunia, jambo lililoacha simanzi kubwa kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.
Tukio hilo limeibua maswali na majonzi makubwa miongoni mwa wanafamilia, huku wakieleza kushtushwa na hali hiyo ambayo hawakuitegemea.