Mwimbaji wa Injili Irene Robert Afariki Ghafla

Global Publishers
March 20, 2026
0 Comments

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Irene Robert, amefariki dunia leo Machi 20, 2026 baada ya kuugua ghafla.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mwimbaji mwingine wa Injili, Walter Chilambo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, akionesha masikitiko kufuatia kuondokewa na rafiki yake wa karibu.

Katika ujumbe wake, Walter amesema marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika huduma ya Injili kupitia muziki, akimtaja kama mtu mwenye moyo wa kujitoa na upendo.

Aidha, imeelezwa kuwa Irene Robert alifariki muda mfupi baada ya kufanya maombi ya muda mrefu usiku.

Irene Robert anakumbukwa kwa nyimbo zake za Injili zikiwemo Neno Moja, Sitolia na Soja.