TMA Yatangaza Tahadhari Ya Mvua Kubwa nchi Nzima Machi 20–21

Global Publishers
March 20, 2026
0 Comments

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya tahadhari na angalizo la mvua kubwa kwa mikoa kadhaa, ikisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari stahiki ili kuepuka madhara yanayoweza kutokana na hali ya hewa mbaya.

Katika taarifa hiyo, TMA imetahadharisha kuwa Ijumaa ya 20 Machi 2026, kunatarajiwa kuwa na mvua kubwa kwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikiwemo visiwa vya Mafia), Tanga, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe, pamoja na visiwa vya Pemba na Unguja.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uwezekano wa kutokea ni mkubwa ikibainisha kuwa athari mbaya zinazoweza kutokea kwa wastani, huku athari zinazotarajiwa zikibainisha mafuriko katika baadhi ya maeneo ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

Kwa Jumamosi ya 21 Machi 2026, TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tabora, Singida na Tanga, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Aidha, Mamlaka hiyo inasisitiza wananchi kuzingatia tahadhari na kujiandaa ipasavyo ili kuepuka madhara yanayoweza kuambatana na mvua hizo.