FCC YAADHIMISHA WIKI YA HAKI ZA MLAJI KWA KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI NJOMBE

Mkuu wa Kanda ya Tume ya Ushindani (FCC) – Nyanda ya Juu Kusini, Bw. Dickson Mbanga,akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia kwa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe (FDC) ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

….

TUME ya Ushindani (FCC) kanda ya Nyanda za Juu Kusini  imetoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe (FDC) kuhusu masuala ya kumlinda mlaji, ikiwemo haki na wajibu wa mlaji pamoja na madhara ya matumizi ya bidhaa bandia katika jamii.

Elimu hiyo imelenga kuwajengea wanafunzi uelewa mpana ili waweze kufanya maamuzi sahihi wanaponunua na kutumia bidhaa mbalimbali  ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Akitoa elimu hiyo Mkoani Njombe, Mkuu wa Kanda ya Tume ya Ushindani (FCC) Nyanda za Juu Kusini, Bw. Dickson Mbanga, amesisitiza umuhimu wa kila mlaji kufahamu haki zake za msingi.alieza kuwa haki hizo ni pamoja na kupata bidhaa bora, kupata taarifa sahihi kuhusu bidhaa, pamoja na haki ya kulalamika pale mlaji anapodhulumiwa.

Aidha, Bw. Mbanga ameeleza madhara makubwa yatokanayo na matumizi ya bidhaa bandia, akibainisha kuwa bidhaa hizo zinaweza kusababisha athari za kiafya, kupoteza fedha, na kudhoofisha uchumi wa nchi. Amewataka wanafunzi kuwa mabalozi wa kuelimisha jamii zao ili kupunguza matumizi ya bidhaa hizo hatarishi.

“FCC imesisitiza kuwa elimu hii ni endelevu na inalenga kuwafikia makundi mbalimbali ya jamii ili kujenga taifa lenye walaji wenye uelewa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.”amesema Bw. Mbanga

Kwa ujumla, mafunzo hayo yameacha alama chanya kwa wanafunzi wa FDC Njombe, ambapo wengi wao wameeleza kuwa elimu hiyo imewafungua macho na kuwapa nguvu ya kusimamia haki zao kama walaji, huku wakiahidi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya bidhaa bandia nchini.

Kupitia mafunzo hayo, walikumbushwa kuwa mlaji ana nafasi kubwa katika kulinda afya yake na uchumi wa taifa kwa kuchagua bidhaa zilizo salama na zenye ubora unaokubalika.

Mkuu wa Kanda ya Tume ya Ushindani (FCC) – Nyanda ya Juu Kusini, Bw. Dickson Mbanga,akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia kwa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe (FDC) ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Mkuu wa Kanda ya Tume ya Ushindani (FCC) – Nyanda ya Juu Kusini, Bw. Dickson Mbanga,akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia kwa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe (FDC) ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Mkuu wa Kanda ya Tume ya Ushindani (FCC) – Nyanda ya Juu Kusini, Bw. Dickson Mbanga,akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia kwa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe (FDC) ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

  Afisa Mlinda Mlaji kutoka FCC Bw.Anderson Lwiza,akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia kwa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe (FDC) ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Sehemu ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe (FDC) Mkoani Njombe wakisikiliza mada mbalimbali wakati wakipata aelimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia yaliyotolewa  na FCC ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.